(Mwanzo 3:9-13)
9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
- Dhambi ni uasi mbele za Mungu /kwenda kinyume na maagizo ya Mungu.
- Kuna zambi za aina mbili (Kutenda usilopaswa kutenda na kuacha kutenda unalopaswa kutenda.
- Kimsingi uhusiano Wetu na Mungu ni imara na mzuri pindi tunapokuwa safi katika hali ya utakaso (utakatifu)
- Dhambi /uasi ni uadui juu ya uhusiano wa binadam na Mungu
- Tunatakiwa kujilinda na dhambi ili kuimarisha uhusiano huu wa Agape.
- MUNGU AKUBARIKI SANA by;evangelistdanielmuyenga@gmail.com
No comments:
Post a Comment